Wednesday, November 22

Utafiti: chaguo la kileo tegemeo la hisia zako

Mvinyo kiasi humfanya mnywaji ahisi kutuliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakati kunywa vinywaji hivyo kwa kiasi inaweza kuwa kiburudisho, watafiti wanatumai matokeo ya utafiti wao yatasaidia kuangazia hatari za unywaji wa vileo wa kupindukia
Aina tofauti za vileo hubadili na kusababisha aina ya hisia za mnywaji kwa namna tofauti, unasema utafiti kuhusu unywaji na hisia.
Vileo vikali kama vile vya aina ya spiriti vinaweza kukufanya uwe mwenye hasira, unaetaka kufanya mapenzi ama mwenye kutokwa na machozi, huku vile vya mvinyo mwekundu(red wine) ama bia vinaweza kukufanya ujihisi mtulivu, wanasema watafiti.
Watafiti hao waliwahoji watu wapatao 30,000 wenye umri wa miaka 18 hadi 34 kutoka mataifa 21 tofauti na kuwasilisha utafiti wao katika jarida la masuala ya afya la BMJ Open.
Waliojibu hoja zao kwa pamoja ni wanywaji wa vileo vya aina ya bia , mvinyo na spiriti, na wengi walisema kuwa kila aina ya kileo kilikuwa na athari tofauti kwao.
Wakati kunywa vinywaji hivyo kwa kiasi inaweza kuwa kiburudisho, watafiti wanatumai matokeo ya utafiti wao yatasaidia kuangazia hatari za unywaji wa vileo wa kupindukia.
Watu hujenga uwezo wa kustahimili kileo kwa muda na hatimae huwa na uwezo wa kunywa zaidi ili kujihisi sawa "athari chanya " kwamba wanaburudika.
Lakini pia wanakabiliwa na hatari ya kupata athari hasi vile vile, alibaini mtafiti Profesa Mark Bellis kutoka Jarida la afya ya umma la Wales.
Utafiti huo unaonyesha utofauti wa vileo hivyo, lakini haufafanui sababu za mabadiliko.
Profesa Bellis anasema mahala kileo kiliponywewa ni kigezo muhimu ambacho kilizingatiwa na utafiti huo ambapo wanywaji waliulizwa kuhusu unywaji wa pombe wa nyumbani na mbali na nyumbani.
Utafiti uliwaangazia watu wapatao 30,000 kutoka nchi mbali mbaliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKulingana na utafiti vijana mara nyingi hunywa pombe aina ya spirit wawapo nje nyakati za usiku
" Vijana walisema mara nyingi hunywa pombe aina ya spirit wawapo nje nyakati za usiku, na hunywa mvinyo zaidi wawapo nyumbani wakitelemshia chakula.
"inatarajiwa pia kuwa my anayetaka kutulia anaweza kunywa glasi ya bia ama ya mvinyo ."
Alisema kuwa utofauti wa namna vinywaji mbali mbali vinavyotangazwa kibiashara na kunadiwa unaweza kuwashawishi watu kuchagua vinywaji vya aina fulani kukidhi hisia zao , lakini hii inaweza kuwa na madhara pale vinywaji hivyo vinaposababisha hisia chanya.

No comments:

Post a Comment