Zaidi ya robo tatu ya wanaume nchini Uingereza wanasema hawajahi au aghalabu wao hudensi, kwa mujibu wa utaifiti wa YouGov survey uliofanyiwa wanaume 1,000 na BBC Radio 5 live.
Kigezo kikuu ni aibu - zaidi ya thuluthi ya wanaume waliohojiwa wanasema wanaona aiu kuingia uwanjani na kunengua viungo.
Asilimia 10 wanasema wanahofia kutazamwa wanapoingia sehemu ya burudani na kuanza kudensi , au kudhihakiwa au kuonekana hawajui kudensi.
Kujiamini
Baadhi ya waliohojiwa wamekiri kuwa hufikiria sana kabla ya kuingia uwanjani au mara nyingine hulewa ili wajihisi vizuri na kujiamini.
"Sidhani kama najua kudensi na kwahivyo, huwa lazima nijipe 'nguvu'kabla ya kuingia uwanjani kudensi," alisema mmoja.
Gareth Dew, mwenye umri wa miaka 35, amekiri yeye hulewa ili apate kujihisi vizuri na kujiamini.
"Kawaida huwa silewi , lakini kama kuna hali ambapo ni lazima ni densi , lazima ninywe glasi kadhaa za whiskey kujituliza roho na kuondosha wasiwasi."
No comments:
Post a Comment