Rais wa Marekani Donald Trump amesema Ijumaa chunguzi mbalimbali zinazofanywa na vyombo vya serikali kuu kuhusu Russia kuingilia kati uchaguzi wa urais ambao ulikuwa na lengo la kumsaidia yeye ashinde ni jambo la "kuaibisha".
Trump pia amedadisi kwa nini wachunguzi hao hawaangazi kuhusu taarifa zilizotolewa kuwa Kamati ya Kitaifa ya chama cha Demokrati ilifanya mambo kinyume cha utaratibu kwa ajili ya kumpendelea mgombea urais Hillary Clinton wakati wa uchaguzi wa awali mwaka jana.
Pia aliuliza maswali kuhusu mgogoro wa DNC katika mtiririko wa tweets kabla ya kuondoka kuelekea kwenye ziara yake ya siku 12 katika nchi za Asia.
Pia aliuliza maswali kuhusu mgogoro wa DNC katika mtiririko wa tweets kabla ya kuondoka kuelekea kwenye ziara yake ya siku 12 katika nchi za Asia.
Tweet hiyo imekuja siku moja baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa mpito wa DNC Donna Brazile alipoeleza kuwa kulikuwa na makubaliano kati ya DNC na kampeni ya Clinton kwamba iliruhusu Clinton kuhodhi fedha za Chama na operesheni nyingine kabla ya uchaguzi kuanza.
“Kila mtu anauliza kwa nini Idara ya Sheria (na FBI) hazichunguzi juu ya vitu vyote vya udanganyifu vinavyoendelea na wadanganyifu Hillary na Chama cha Demokrat…”
Katika ujumbe wake wa pili wa tweet, Trump alitaja taarifa iliyotolewa na Brazile, ambayo iliandikwa katika kitabu chake kipya, na kutaja mambo mengine kadhaa yanayomzunguka Clinton na DNC.
“…Kitabu kipya cha Donna B Book kinasema alilipa na kuiba katika uchaguzi wa awali. Na vipi kuhusu barua pepe alizozifuta, Uranium, Podesta, Server ya kompyuta, n.k, n.k…”
Na katika tweet nyingine, Rais alielekeza mazungumzo yake kwa wachunguzi wa serikali kuu, ambao alikuwa amedai kuwa hawafanyi kazi yao ipasavyo.
“Watu wanahasira. Kwa namna fulani Idara ya Sheria na Shirika la Upelelezi la FBI, lazima wafanye lile lililo sahihi na linalostahili. Umma wa Wamarekani unastahili kutendewa haki.”
Trump alikusudia katika tweet yake ya nne kuwa madai yanayotolewa siyo ya kweli kwamba kampeni yake ya urais ilishirikiana na Russia kuingia ikulu ya White House mwaka jana.
“Habari ya uhakika kuhusu udanganyifu huo iko katika kitabu kipya cha Donna B. Mdanganyifu Hillary aliwanunua DNC na baadae kuiba chaguzi za awali kupitia kwa mwendawazimu Bernie."
No comments:
Post a Comment