Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbiliny (Sugu) akichukua matukio kwa kutumia simu yake, wakati wakisubiri kutangaziwa matokeo ya uchaguzi Kata ya Ibighi Wilaya ya Rungwe, Mbeya. Matokeo yanatangaziwa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ibighi. Picha na Godfrey Kahango.
Chalya amefika muda mfupi leo Jumapili jioni baada wasimamizi kutoka vituo vyote vya kupigia kupeleka maboksi ya kura katika Ofisi ya Kata ya Ibighi kwa ajili ya kujumlishia kura.
Baada ya kuingia ndani Chalya ndipo Sugu na Mwakagenda nao wakaingia ndani ambapo wametolewa nje na Mkuu wa Kituo cha Polisi(OCD) Rungwe kwa madai hawahusiki na wanaohusika ni wagombea na mawakala wao.
Sugu na Mwakagenda wakaibua hoja kwamba mkuu huyo wa Wilaya kwamba naye anatakiwa kutoka na si vinginevyo.
“Sawa tunatoka lakini na huyo Mkuu wa Wilaya anatafuta nini ndani? Naye atoke ili turidhike wote," amesema Sugu.
Baada ya kauli hiyo, OCD amesema 'isiwe shida naye anatoka tu'. Kweli Chalya ametii hilo na kutoka nje taratibu.
No comments:
Post a Comment