Rais wa Nigeria Mohammadu Buhari ameunga mkono mpango wa kuwafuta kazi zaidi ya walimu 20,000 ambao walifeli mitihani katika jimbo la kaskazini la Kaduna.
Buhari aliitaja hali hiyo ku mbaya.
"Ni jambo la kusikitisha kuwa wakimu hawezi kupita mitihani ambayo wanastali kuwafunza watoto, ni jambo baya sana."
Gavana wa jimbo hilo wiki iliyopita alichapissa makaratasi yaliyuwa yamesahihishwa kwenye mtandao wa Twitter akisema kuwa walimu hao walikuwa wamefeli mtihani kwa darasa la nne ambao unastahili kufanywa na wanafuzi wa umri wa miaka 10.
Alisema kuwa walimu hao watafutwa lakini wanaweza tena kutuma maombi katika shughuli mpya ya kuwaajiri walimu ikiwa wanahisi wana ujuzi unaostahili.
Msemaji wa gavana Samuel Aruwan aliiambia BBC kuwa shughuli hiyo itakamilika mwezi Februari mwaka 2018.
Alisema kuwa maombi ya kazi 19,000 yamepokelewa kuchukuaa mahala pa walimu hao ambao hawakupata hata alama 75 kwenye mtihani huo.
Vyama vya wafanyakazi hata hivvyo vimepinga hatua hiyo ya kuwafuta walimu.
No comments:
Post a Comment