Thursday, November 23

Polisi walifunga jarida la Red Paper nchini Uganda

Jarida la Red Paper nchini Uganda lafungwaHaki miliki ya pichaRED PAPER
Image captionJarida la Red Paper nchini Uganda lafungwa
Polisi nchini Uganda wamelifunga jarida moja kubwa zaidi la habari za udaku The Red Pepper, na kuwatia mbaroni baadhi ya wafanyikazi wake.
Wakurugenzi wakuu watano wa gazeti hilo wanazuiliwa na polisi, kwa pamoja na wahariri kadhaa.
Hii inafuatia taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo, inayodai kuwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni alikuwa akipanga njama za kupindua utawala wa Rwanda.
Madai hayo yamekanushwa na serikali ya Uganda.
Katika siku kadhaa za nyuma, Gazeti hilo la Red Pepper, limewahi kukumbwa na utata kadhaa.

No comments:

Post a Comment