Thursday, November 23

Nelly kutumbuiza katika tamasha la wanaume pekee Saudia

Nelly kushiriki katika tamasha la wanaume pekee Saudia
Image captionNelly kushiriki katika tamasha la wanaume pekee Saudia
Ni mpango unaotarajiwa kuunganisha mashariki na magharibi kupitia muziki lakini badala yake unawagawanya wanaume na wanawake nchini Saudia.
Nyota wa muziki wa hipo hop Nelly na mwimbaji wa Algeria Cheb Khaled wanatarajiwa kushiriki katika tamasha moja la muziki huko Jeddah mnamo tarehe 14 mwezi Disemba.
Lakini tamasha hilo litahudhuriwa na wanaume pekee na ijapokuwa wale watakaohudhiria ni wengi mno baadhi ya wanawake nchini humo wamekasirishwa na hatua hiyo.
Katika mitandao ya kijamii walihoji ni kwa nini wanatengwa katika tamasha hilo lililoandaliwa na runinga moja ya kibinafsi MBC Action na kuungwa mkono na mamalaka ya burudani nchini humo.
Wengine wamedai kwamba baada ya rapa huyo kuhudumia kifungo jela kwa kutumia bangi 2015 mbali na kushtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia mwezi uliopita hafai kuruhusiwa kushiriki katika tamasha hilo.
Licha ya kushtakiwa kwa kumiliki dawa za kulevya ,ambapo hakuhudumia kifungo jela, Nelly amekana madai ya ubakaji yaliowasilishwa na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na hajashtakiwa.

No comments:

Post a Comment