Mwanamke aliyepigwa picha akiuonyesha msafara wa rais Donald Trump ishara ya kidole cha kati ameripotiwa kufutwa kazi na kampuni iliomuajiri kufutia picha hiyo.
Picha hiyo ilisambazwa baada ya kupigwa mnamo terehe 28 mwezi Oktoba mjini Virginia karibu na uwanja wa kucheza Gofu wa Trump.
Juli Briskman ambaye alitambulika kama mwendesha baiskeli anadai kwamba alifutwa kazi na mwajiri wake Akima LLC baada ya kuichapisha katika mtandao wake.
Kampuni hiyo hatahivyo haikutoa tamko lolote ilipotakiwa kufanya hivyo na BBC.
Bi Briskman aliambia vyombo vya habari kwamba kampuni hiyo ilimuita katika mkutano siku moja baada ya kumwambia afisa mkuu wa ajira kwamba ni yeye ndiye aliyepiga picha hiyo.
- Mbona wanamuziki wamempuuza Trump?
- Kanye hatatumbuiza sherehe ya Trump
- Melania ajibizana na mke wa zamani wa Trump
Alilimbia gazeti la Huffington Post kwamba maafisa wakuu wa kampuni hiyo walimwambia kwamba picha hiyo imeorodheshwa kama chafu na kwamba ilikiuka viwango vya sera za mitandao baada ya kuichapisha katika akaunti zake za Twitter na facebook.
Hatahivyo bi Briskman alisema kuwa aliusisitizia usimamizi wa kampuni hiyo kwamba hakuwa akifanya kazi wakati picha hiyo ilipopigwa na kwmaba hakuwataja waajiri wake katika mtandao huo wa kijamii.
Bi Briskman anasema kuwa mwenzake wa kiume hakufutwa kazi baada ya kufuta picha iliodaiwa kuwa chafu katika kisa chengine.
Hivyobasi amekuwa akihoji ni kwa nini alifutwa kazi mara moja.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 ambaye ana watoto wawili ameripotiwa kufanya kazi katika kampuni hiyo ya serikali kwa miezi sita akifanya kazi ya mawasiliano.
No comments:
Post a Comment