Serikali imewasilisha Mus-wada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma 2017 ambao ukipitish-wa, wanachama wake wanaotaka kujitoa watakabiliwa na masharti makali huku ukiruhusu mtoto mle-mavu kuendelea kulipwa kwa mai-sha yake yote.
Pamoja na mapendekezo mengi yaliyomo, muswada huo umeweka masharti kwa kwa watumishi wanaostahili kulipwa kabla hawa-jatimiza umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 55 kwa hiyari au 60 kwa lazima.Atakayetaka kujitoa, muswada unamtaka awe na “cheti cha dak-tari kwamba hawezi kuendele akutekeleza majukumu yake amba-cho mwajiri wake atakiridhia au ajira yake ikisitishwa kwa maslahi ya umma au muda wake wa uteuzi utakapokamilika.”Muswada unaongeza masharti kwamba, mwanachama yeyote atastahili mafao endapo atakuwa amechangia walau miaka 15 au jum-la ya miezi 180.Mfuko unawatambua watoto na mwenza wa kila mwanachama. Kwa uzito uliopo, unapendekeza kum-lipa mtoto mlemavu wa mwana-chama atakayepoteza maisha akiwa kazini kwa maisha yake yote yali-yobaki wakati ambao ni wazima, mpaka watakapotimiza miaka 21.Wakati mtoto ikipendekezwa apewe mafao hayo, mjane naye, kul-ingana na umri na watoto alioachi-wa, amezingatiwa. Kwa aliyeachwa na watoto wenye chini ya miaka 15 naye akiwa na zaidi au chini ya miaka 45, muswada unapendekeza alipwe mafao kwa maisha yake yote au mpaka atakapoolewa tena.Endapo mwanachama hakuacha mtoto wala mke, inapendekezwa: “Wazazi wake walipewe haki zote za mtoto wao.”
Kutekeleza mabadiliko hayo, muswada unapendekeza kuvunjwa kwa mifuko ya PPF, GEPF, LAPF na PSPF kasha kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) utakaorithi mali na madeni yote ya mifuko hiyo iliyopo sasa.
Itakapopitishwa, kutakuwa na kipindi cha mpito cha miezi sita kukamilisha hatua zote za kisheria zinazohitajika kabla utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo mpya utakaokuwa na thamani ya Sh5 trilioni haujaanza.
Mabadiliko hayo yataiacha mifuko minne kutoka saba ya sasa ukiwamo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wakati PSSSF ukiwahudumia watumishi wa umma, NSSF utakuwa kwa ajili ya sekta binafsi.
Kwenye makabidhiano yatakayofanywa, michango na wanachama wa NSSF ambao ni watumishi wa umma watahamishiwa PSSF wakati wale wa sekta binafsi kutoka huko watahamishiwa NSSF. Wafanyakazi wenye sifa wa mifuko itakayovunjwa wataajiriwa PSSSF itakayochukua madeni na mali za mifuko hiyo pia.
Utafiti wa ajira na kipato wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) mwaka 2015 unaonyesha kuna watumishi milioni 2.3 nchini ambao kati yao, milioni 1.6 wanatoka sekta binafsi na 700,000 ni wa umma.
Mfuko huo utatoa mafao manane ambayo ni la kustaafu, warithi, kujitoa, uzazi na kutokuwa na ajira. Mengine ni fao la ugonjwa, kifo na mzishi.
Sharti limewekwa kwamba: “Haitaruhusiwa kwa mwanachama kupewa mafao mawili kwa wakati mmoja.”
Wanachama
Muswada unapendekeza wanachama kuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa nyumba kwa dhaman ya michango yao waliyonayo kwenye mfuko huu mpya. Vilevile, wanaochangia kwa hiyari kwenye mifuko minne itakayofutwa watahamishiwa PSSSF.
Muswada unashauri, mafao ya mwanachama yanaweza yakatumika kulipa deni la serikali, mkopo wa nyumba au malezi na matunzo ya mtoto au mke aliyetelekezwa baada ya kujiridhisha kwa mamlaka husika.
Kukabiliana na ucheleweshaji wa malipo ya mafao kwa wastaafu, muswada unapendekeza itakapodhihirika kuwa ucheleweshaji huo haukuchangiwa na mtumishi husika basi mfuko umlipe mafao yake pamoja na riba ya asilimia tano ya thamani ya mafao yake kwa mwaka.
Suala la makosa yanayoweza kuhumiwa kifungo gerezani, muswada unapendekeza wategemezi wake; mke na watoto walipwe stahiki za mtumishi husika ili waweze kujikimu kwa muda ambao mwanachama huyo atakuwa anatumikia kifungo chake.
Kwa mwanachama atakayehukumiwa kifungo lakini hana wategemezi, pindi hukumu yake ikiisha, mfuko unawajibika kumlipa mafao yake yote anayostahili kwa muda aliochangia.
Ikitokea mfanyakazi wa umma amebadili mwajiri na kwenda sekta binafsi, uanachama wake utahamishiwa NSSF lakini michango yake itaendelea kubaki PSSSF na muda wa kustaafu utakapofika au sababu nyingine ya kulipwa mafao yake, ukokotozi wa pamoja utafanywa kati ya mifuko hiyo miwili.
Jambo jingine muhimu kwenye muswada huo ni madai yaliyotelekezwa. Inapendekezwa, mwanachama ambaye warithi wake hawatajitokeza kwa miaka mitatu mfululizo kufuatilia michango yake kutokana na kifo au sababunyingine yoyote, kiasi kilichopo kitahamishiwa kwenye akaunti maalumu ya serikali.
Na hali ikiendelea kuwa hivyo kwa miaka 10, akaunti ya mwanachama itafutwa na fedha zake kuhamishiwa serikalini.
Mali, madeni
Muswada unatambua watumishi wa mifuko inayotarajia kuunganishwa, mali za taasisi hizo, madeni pamoja na miradi mbalimbali. Muswada unapendekeza kwamba, mikataba yote iliyopo ambayo inaendele akutekelezwa kuhamishiwa PSSSF.
Uhamisho huo pia utahusisha mali na madeni yaliyopo bila kusahau miradi. Haya yote yanatakiw ayafanywe ndani ya miezi sita ambayo ni kipindi cha mpito kwa ajili ya makabidhiano.
Hesabu za fedha
Ndani ya miezi sita baada ya kukamilika kwa mwaka wa fedha, bodi ya wakurugenzi ya PSSSF italazimika kuandaa hesabu za fedha na ripoti yake kuiwasilisha kwa waziri mwenye dhamana ambaye atawajibika kupeleka nakala na kuisoma bungeni.
Bodi itatakiwa kutoa ripoti hizi kila mwaka ambazo zitajumuisha taarifa za mali na madeni, operesheni za mfuko, matumizi ya fedha za mfuko na taarifa nyingine yoyote ambayo waziri au mamlaka za juu zaidi zitahitaji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA), Irene Isaka anasema mapendekezo haya yamefanywa baada ya tathmini ya kina iliyozingatia mambo mengi yaliyoshauriwa na vyama vya wafanyakazi.
Kukamilisha mchakato huo, Isaka anasema tahadhari inachukuliwa kuhakikisha watumishi waliopo hawapotezi kazi zao. Kwa waliopo ngazi za ukurugenzi, alisema wanaweza kupangiwa majukumu mengine endapo itaonekana nafasi zao zimejaa kwenye mfumo huu mpya.
“Hii sekta bado inahitaji wafanyakazi wengi kukidhi mahitaji yaliyopo na yanayoongezeka kila siku. Hatma ya wafanyakazi waliopo kwenye mifuko inayounganishwa itafahamika baada ya muda mfupi,” anasema.
Kuhakikisha mambo yanaenda sawa, anasema Wizara ya Utumishi inashughulikia suala hilo hasa kwa kutambua kwamba baadhi ya mifuko ilikuwa na wafanyakazi wengi kuliko mahitaji ilhali mingine ilikuwa nao wachache hivyo, kama watakuwapo watakaopoteza nafasi zao, hawatokuwa wengi.
Licha ya mustakabali wa watumishi waliopo, anasema wizara hiyo pia inaandaa mfumo sahihi utakaowahudumia waajiriwa waliopo sekta binafsi pamoja na wale wa sekta ya umma.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya HakiPension, Christian Gaya anasema muungano huo utakuwa mzuri endapo wananchi wengi zaidi watakuwa na nafasi ya kujiunga na huduma za hifadhi ya jamii na mmafao kutolewa kwa wakati. “Kwa sasa mafao ya wafanyakazi yanacheleweshwa ilhali kuna mifuko mingi yenye ushindani. Sijui itakuwa kutakapokuwa na mifuko miwili pekee,” anatia shaka Gaya.
No comments:
Post a Comment