Miaka saba iliyopita Amol Yadav alitangaza kwa familia yake na marafiki kuwa angejenga ndege kwenye paa la nyumba yao katika mji wa Mumbai India.
Familia na marafiki waliokua wamepigwa na butwa walimuuliza rubani huyo ni vipi angeweza kuishukisha ndege ikikamilika
"Kwa uhakika sijui," aliwajibu.
Bw Yadav ni rubani wa ndege za kutumia injini mbili.
Walijikakamua kupandisha vifaa vya kuijengea ndege hiyo hadi paa la nyumba ya familia la ghorofa tano, ikiwemo injini iliyonunuliwa kutoka ng'ambo ya zaidi ya kilo 180.
Mwezi Februari mwaka uliopita, ndege hiyo ya injini moja yenye nafasi ya watu 6 ilikuwa imekamilika.
Kulingana na Bwa Yadavm, ndege hiyo ndiyo ya kwanza kujengewa nyumbani nchini India.
Anasema kuwa injini hiyo ina nguvu za kuiwezesha ndege hiyo kupaa umbali wa futi 13,000 na tanki lake linaweza kubeba mafuta ya kuiwezesha ndege hiyo kusafiri umbali wa kilomita 2000 kwa kasi ya kilomita 342 kwa saa.
Serikali ilikuwa imeandaa maonyesho ya vifaa vilivyotengenezwa chini India mji Mumbai.
Wakati Yadav aliomba ruhusa kutoka kwa waandalizi kuonyesha ndege yake, walikataa wakisema kuwa hakukuwa na nafasi ya kutosha. Ilibidi ndugu wake wang'ang'a kutafuta nasafi.
"Kwa hivyo tuliamua kuobomoa ndege hiyo ili tuishukishe kwa sehemu tofauti na tuipeleke kwa maonyesho kwa lazima na kuionyeha kwa dunia, Bw Yadav alisema.
Waliibomoa ndege na kutenganisha injini, mkia na mabawa na kuishukisha kwa kutumia kreni.
Sehemu hizo ziliwekwa kwenye lori na kusafirishwa huku sehemu nyingine ikivurutwa na gari ndogo umbali wa kilomita 25.
Waliruhusiwa kuingia kwa maonyesho ambapo yeye na mafundi wake waliiunganisha ndege hiyo kwa muda wa saa tatu.
Wakati maonyesho yalianza ndege hiyo iliwavutia watu wengi.
Gazeti moja liliandika taarifa hiyo hali iliyochangia wageni wengi kufika akiwemo waziri wa safari za ndege wa India na wafanyabiashara.
Bwana Yadav sasa anasema kuwa yuko tayari kujenga ndege ya kwanza kabisa kujengwa India.
Wawekezaji wameonyesha moyo wa kuwekeza na serikali ya BJP imeahidi kumpa ekari 157 za ardhi za kujenga kiwanda cha kuunda ndege za kubeba abiria 19.
No comments:
Post a Comment