Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC huko The Hague, imewaamrisha waendesha mashtaka kuanzisha uchunguzi kamili kuhusu madai ya uhalifu dhidi ya binadamu ulitokea nchini Burundi.
Majaji walisema kuwa kuna sababu za kuchunguza uhalifu huo ukiwemo mauaji na mateso uliofanywa na serikali na makunde yenye uhusiano na serikali.
- Burundi yajiondoa rasmi katika mahakama ya ICC
- Raia wa Burundi ''waliotaka kujiunga na al-Shabab'' wakamatwa
Burundi ilijiondoa kutoka ICC mwezi uliopita lakini mahakama ya ICC inasema kuwa inaweza kuchunguza uhalifu ulitokea hadi wakati huo.
Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa mamia ya watu waliuawa wakati wa ghasia zilizoibuka baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment