Ni jina la mahoteli ya kifahari yaliyo maarufu kote duniani.
Marais, mawaziri wakuu na wafalme wamekaribishwa katika mahoteli ya Ritz-Carlton.
Lakini kwa mujibu wa ripoti kadhaa, mahoteli hayo katika mji mkuu wa Saudi Arabia yamekuwa gereza.
Miezi michache baada ya kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa ziara yake ya kwanza kama rais, watu kadhaa mashuhuri nchini Saudi Arabia sasa wanaripotiwa kuwa wageni wa serikali huku hoteli hiyo ikitajwa kuwa gereza la kifahari zaidi duniani.
Wanawafalme 11, mawaziri wanne na watu wengine kadhaa wamekamatwa katika kile mamlaka za saudi Arabia zinasema kuwa ni kampeni ya kupambana na ufisadi nchini humo.
Bilionea maarufu duniani Prince Alwaleed bin Talal anaripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliokamatwa.
- Wana wa ufalme wakamatwa Saudi Arabia
- Kombora larushwa karibu na uwanja wa ndege Saudi Arabia
- Wanawake kuruhusiwa kuingia viwanja vya michezo Saudi Arabia
Mtandao wa gazeti la The New York Times ulichapisha kanda ya video iliyoonyesha wajibu mpya wa hoteli ya Ritz-Carlton Riyadh.
Katika video hizo walinzi wanaonekana wamelala kwenye mikeka katika chumba kimoja cha hoteli, watu wenye sare pia nao wanaonekana huku bunduki zikionekana zikiegeshwa kwenye ukuta.
Gazeti la Guardian liliripoti kuwa wageni waliombwa siku ya Jumatano jioni wakusanyike sehemu moja na mizigo yao, kabla ya kusafirishwa kwenda kwa hoteli zingine mjini Riyadh.
The Guardian inamnukuu afisa mmoja wa Saudi Arabia akisema kuwa mamlaka hazingeweza kuwaweka watu hao gerezani na hilo lilikuwa suluhu bora.
Jitihada za kulipia vyumba katika hoteli hiyo siku ya Jumannwe hazikuzaa matunda.
No comments:
Post a Comment