Mahakama moja mashariki mwa India imemhukumu mwanamume mmoja wa Bangladesh kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtawa mwenye umri wa 71 mnamo mwezi Machi 2015.
Mahakama hiyo ya Kolkata ilimpata Nazrul Islam na makosa ya ubakaji na jaribio la mauaji.
Watu wengine watano walihukumiwa jela kwa miaka 10 kwa wizi wakati wa kisa hicho mjini Ranaghat, magharibi mwa jimbo la Bengal.
Mtu mwengine wa sita alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kuwaficha watu hao.
Bibi huyo mwenye umri wa miaka 71 alishambuliwa baada ya wezi hao kupora nyumba yake.
Wezi hao waliiba fedha na vifaa vyengine wakati wa shambulio hilo ambalo liliwashangaza watu wengi nchini India na kusababisha maandamano.
''Kile kilichomfanyikia mtawa huyo mwenye umri wa miaka 71 ni janga kwa sifa za jimbo la West Bengal ambapo Mama Teresa aliwafanyia kazi watu masikini'', jaji Kumkum Singha aliiambia mahakama iliojaa watu siku ya Jumatano.
Mtawa huyo ambaye hakutajwa jina lake kwa sababu za kisheria alifanyiwa upasuaji baada ya kitendo hicho kilichofanyika katika nyumba ya Jesus na Mary.
Baadaye aliondolewa katika eneo hilo.
Taifa la India limekuwa likishuhudia visa vingi vya mashambulizi katika makanisa miongoni mwa jamii ndogo ya Wakristo.
Mamlaka pia imeimarisha sheria zake za unyanyasaji wa kijinsia kufuatia kubakwa kwa mwanafunzi wa shule hadi kufa katika mji mkuu wa Delhi 2012.
Hatahivyo, wanaofanya kampeni wanasema kuwa mashambulizi kama hayo yametapakaa.
No comments:
Post a Comment