Tuesday, October 10

ZANZIBAR

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFURAHIA HUDUMA ZA NHIF KATIKA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA NA UZIMAJI WA MWENGE YANAYOENDELEA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA AMAAN - ZANZIBAR.

Katika maonesho ya Wiki ya Vijana na Uzimaji wa Mwenge Makamu wa Rais wa pili Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maonesho hayo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kutoa Elimu bure kwa wananchi wa Zanzibar kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kama Shinikizo la Damu (BP), Sukari na uwiano wa Uzito na Urefu, lakini pia kwa upimaji wa magonjwa hayo bure.

Alisisitiza NHIF isiishie kwenye Maonesho hayo lakini iwe ikitoa huduma hiyo mara kwa mara pindi Mfuko upatapo fursa ya kufanya hivyo, vilevile Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Mfuko na Fao jipya la TOTO AFYA KADI kwani gharama yake ni nafuu, tofauti na gharama za matibabu ya afya mahospitalini aliuasa Mfuko uhamasishe fao hilo ili watu waweze kujiunga kwa wingi, kwani watoto ni Taifa la kesho, ili waweze kufikia malengo yao wanahitaji uhakika wa Afya zao.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaendelea kuwakaribisha wananchi wazidi kujitokeza kwa wingi kuja kupima afya zao bure na vilevile kujiunga fao la Toto Afya Kadi, "Mfuko umejipanga kuhakikisha kila mwananchi anakua na kadi ya Bima ya afya, kwani ili kua na Taifa lenye maendeleo linahitaji wananchi wenye uhakika na huduma za Afya na Mfuko uko kwa ajili ya kuhakikisha hilo" alisema Meneja wa NHIF Zanzibar Bw. Ismail Kangeta.

Wiki ya Vijana inaadhimishwa kuanzia tarehe 8/10/2017 hadi tarehe 14/10/2017 kama sherehe ya Kumbukumbu ya hayati Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere.
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akielezewa jambo na Meneja wa NHIF Zanzibar Bw. Ismail Kangeta pindi alipotembelea banda la NHIF baada ya kufungua Rasmi Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Amaan.
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akicheki afya kwenye banda la NHIF, katika Maonesho ya Wiki ya Vijana.
Afisa wa NHIF Bw. Shabani Muhunzi akielezea jambo kwa mdau alietembelea banda la NHIF kwenye viwanja vya Amaan Zanzibar kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana.
Afisa Matekelezo wa NHIF Zanzibar Bi.Naima Aboubakar akiwaelezea vijana waliokuja kutembelea banda la NHIF kuhusiana na Huduma zitolewazo na Mfuko huo.

No comments:

Post a Comment