Thursday, October 12

YASEMEKANA TECNO KUJA KIVINGINE


Kwa hiyo inasemakana kaka wa wale wapenzi wawili, Mnyama yuko njiani kuja. Ndio umesikia sahihi, kizazi kifuatacho cha muendelezo wa Phantom kipo njani kutufikia. Shangwe kwa mfalme!
Japo habari ni kuwa #Lejendari yupo njaini kufika ila natamani hii simu ingetoka mwezi huu October, tukiachana na hayo kuna mambo machache ambayo ningetamani TECNO wayafanye, wayaongeze na kubadilisha. Pia nasikia itaiwa PHANTOM,( nambie mtazamo wako)

Tukitazama nyuma, Phantom 6 plus battery yake inauwezo wa 4050mAh, na kiukweli, tukubaliane ni inakidhi kwa matumizi ya siku nzima na Zaidi, na juu ya yote kasi ya kuchaji simu. Yani Simu ina mfuma wa “Fast charging” na pia battery yake inakaa muda mrefu, bomba kabisa!
Ila ningependa kuwaomba TECNO, pamoja na kuleta mnyama round hii kuna baadhi ya vitu ningependa kuviona kutoka kwenye hii simu mpya, na mimi binafsi nisingependa kuona uwezo wa battery ukiwa chini ya mAh 4000, yaani haitaleta mantiki, yaani kiaje kwa mfano?, tuko kwenye karne ya simu janja ambapo zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku, sisi kama watumiaji wa simu katika kufanyia mambo mengi tofauti hatutopenda kuoa notification ya “LOW BATTERY” hata siku haijaisha.

 Natumaini kwenye hii simu ijayo mtaweka kasi kwenye mfumo wa kuchaji, kuchaji ndani ya 45 labda? Sijui lakini, itakua surprise sana mkifanya hivyo!
Lakini pia, hiyo isiwe shida wakati wote kama Phantom inayofuata itafanya  vizuri ili kuunganisha vizuri betri na programu.

Baada ya kuzungumza sana ni hayo tu wadau wa smartphones, kaka mkubwa yuko njiani. Na unaweza kuanza kukaa mkao wa kula kwani itakua ya kilejendari.

No comments:

Post a Comment