Watu 40 wameuwa na mamia ya wengine hawajulikani waliko baada ya siku sita za moto wa nyika ambao umeharibu maeneo makubwa ya ardhi katika jimbo la California nchini Marekani.
Gavana wa California anasema kuwa ni moja ya majanga makubwa zaidi jimbo hilo halijawahi kushuhudia.
Zaidi ya wazima moto 10,000 wanapambana na karibu mioto 16 iliyozalia.
Upepo unaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 70 ulisababisha moto huo kusambaa zaidi na kulazimu watu zaidi kuhama.
Moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni mji wa Santa Rosa ambapo hadi watu 3000 walihamishwa siku ya Jumamosi.
"Uharibifu ni mkubwa," Gavana Jerry Brown alisema alipofaya ziara katika mji huo.
Huo ndio moto mbaya zaidi katika historia ya jimbo hilo. Zaidi ya watu 100,000 wamehamishwa na vijiji vingi vimegeuka majivu
Moto huo mkubwa umesababisha moshi na majivu hadi anga ya San Francisco, karibu umbali wa maili 50, na hata kwenda miji ya mbali kusini.
Katika bonde na Naqa takriban viwanda 13 vya mvinyo vimeharibiwa. .Mmiliki mmoja wa kiwanda cha mvinyo huko Santa Rosa anasema moto huo umeharibu mviyo wa mamilioni ya dola.
No comments:
Post a Comment