Wakuu hao wa mikoa, Christopher Ole Sendeka (Njombe) na Amos Makalla (Mbeya) kwa nyakati tofauti pia kila mmoja alitoa kilio chake mbele ya waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba. Dk Tizeba aliteuliwa hivi karibuni kuwa waziri wa wizara hiyo mpya iliyomegwa kutoka ile ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (Sagcot) kwa mikoa ya Mbeya na Songwe, Sendeka alisema atasimamia maagizo hayo na kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora ili waweze kuzalisha mazao yenye tija na kufanikisha azma ya Serikali.
Kwa upande wake, Makalla alimuomba waziri huyo kufanya kila linalowezekana kuongeza idadi ya maofisa ugani kwa kuwa mkoa wake una upungufu wa zaidi ya watumishi hao 850 hali inayofanya wakulima kutofikiwa kwa wakati.
Awali, waziri Tizeba aliwaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuendeleza mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa mazao ya mahindi na mpunga ili kuwawezesha wakulima kuacha kutegemea mvua. “Wakuu wa mikoa sasa nimewaachia mpira huo muucheze mhakikishe mnawatumia maofisa kilimo kuweka mikakati na kuona namna ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji katika mazao yaliyo na tija na kuwezesha kuingiza katika mnyoyoro wa thamani,” alisema.
No comments:
Post a Comment