Uchaguzi nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo hautafanyika hadi mwezi Aprili mwaka 2019, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchi humo.
Katika taarifa tume ilisema kuwa inahitaji takriban siku 504 kuweza kuandaa uchaguzi huo mara usajili wa wapiga kura utakapokamilika
Hii ni kinyume kabisa na makubaliano kati ya Rais Joseph Kabila na upinzani, ulioongozwa na kanisa katoliki kuwa uchaguzi ungefanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
- Kuahirishwa uchaguzi DRC 'huenda kukazusha ghasia'
- DRC haina fedha za uchaguzi wa rais
- Mtandao kubanwa DRC
- Mhubiri kutoka DRC apewa hifadhi Afrika Kusini
Uchaguzi ulipangwa kufanyika Novemba mwaka 2016, lakini ukafutwa na tume ya uchaguzi kutokana changamoto za usafiri na za kifedha.
Hii ina maana kuwa Rais Joseph Kabila amekaa madarakani kinyume na muda unaostahili kisheria.
Watu kadhaa waliuawa wakati wa maandamano.
Kulingana na shirika la habari la Reuters, mapigano katika eneo la Kasai yamechelewesha shughuli ya usajili wa wapiga kura.
No comments:
Post a Comment