Friday, October 27

Trump aamrisha kutolewa kwa siri za mauaji ya JF Kennedy

Rais wa zamani wa Marekani John F Kennedy
Image captionRais wa zamani wa Marekani John F Kennedy
Rais Donald Trump wa Marekani, ameamrisha idara ya kitaifa ya kuhifadhi kumbukumbu, kutoa zaidi ya stakabadhi elfu tatu, yanayohusishwa na mauaji ya aliyekuwa Rais wa Marekani John F. Kennedy aliyeuwawa, zaidi ya nusu karne iliyopita.
Rais Kennedy aliuwawa mwaka 1963.
Ikulu ya White imesema kuwa mamia ya faili zilizo na taarifa nyeti, hazitawekwa hadharani mwezi Aprili mwakani, baada ya mashirika ya ujasusi, CIA na FBI kukataa zitolewe.
Rekodi hizo, kwa sasa zimechapishwa kwenye tovuti ya mtandao wa idara ya kitaifa ya Marekani inayohifadhi kumbukumbu.
Swali kuwa, muuwaji wa rais Kennedy, Lee Harvey Oswald, alitenda mauaji hayo kivyake ama alitumwa na watu au kundi fulani, bado ni fumbo ambalo halijafumbuliwa hadi sasa, huku vitabu, majarida na hata filamu zikitolewa kuhusiana na mauaji yake.

No comments:

Post a Comment