Thursday, October 12

Siri za kijeshi za Australia zaibwa kupitia udukuzi

Ndege ya kijeshi aina ya F-35 iliokuwa katika mpango wa kijeshi wa taifa hiloHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNdege ya kijeshi aina ya F-35 iliokuwa katika mpango wa kijeshi wa taifa hilo
Habari za siri kuhusu mpango wa jeshi la serikali ya Australia zimeibwa katika udukuzi wa mtandaoni.
Takriban GB 30 za data zilizokuwa na mwanakandarasi wa serikali zilidukuliwa ,ikiwemo maelezo kuhusu ndege mpya za kijeshi na manuwari.
Data hiyo ilikuwa na siri kubwa lakini haikutajwa kiwango chake kulingana na serikali hiyo.
Maafisa wa kukabiliana na maswala ya usalama wa mitandaoni nchini Australia walimtaja mdukuzi huyo kwa jina 'Alf' baada ya jina la muigizaji wa kipindi cha runinga cha 'Home and Away'.
Udukuzi huo ulianza mnamo mwezi Julai mwaka uliopita lakini idara ya ishara nchini Australia haijkujulishwa hadi mwezi Novemba.
Mdukuzi huyo hajulikani.

No comments:

Post a Comment