Monday, October 9

Rais Trump atangaza matakwa yake ya mabadiliko ya sheria za uhamiaji

Rais Donald Trump wa Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump aliweka wazi Jumapili kwamba ili kufikia makubaliano na wademocrat kuruhusu wale wahamiaji wanaofahamika kama 'Dreamers' kuendelea kukaa Marekani, atashinikiza kurekebisha mfumo kamili wa kibali cha ukaazi maarufu kama 'Green Card' akitaka kuajiri maafisa wa uhamiaji zaidi ya 10,000 na kujenga ukuta kwenye mpaka wa kusini.
Mwezi uliopita Rais Trump alitangaza mpango wa kufutilia mbali mradi wa Deferred Action for Childhood Arrivals-DACA, sera ya enzi ya utawala wa rais wa zamani Barack Obama ambayo inawalinda maelfu ya vijana ambao waliingia nchini kama watoto kinyume cha sharia.
Sera ya uhamiaji ya Rais Trump inajumuisha kupunguza kuwapatia wake na watoto wa mtu mwenye kibali cha ukaazi halali yaani Green Card au kwa raia wa Marekani, na badala yake kubuni mfumo wa kutoa natija kwa ajili ya jamaa hao. Lakini wademocrat mara moja wamepinga vikali matakwa hayo ya rais.

No comments:

Post a Comment