Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jumuiya ya Ulaya, Federica Mogherini, amekosoa matamshi ya Bwana Trump ya kutaka kujiondoa katika mapatano ya nyukilia na Iran.
Alisema kuwa hakuna Rais yeyote mwenye mamlaka ya kuangamiza mapatano yaliyoidhinishwa na baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Alisema mapatano hayo ni muhimu zaidi wakati huu ambapo hatari ya zana za kinyukilia imeonekana dhahiri.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Urusi imesema kuwa imesikitishwa na msimamo wa Rais Trump lakini lakini ikafafanua kuwa haitarajii hatua yake kusababisha mabadiliko makubwa katika mkataba huo.
Waziri Mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu, alimpongeza Rais Trump katika kile alitaja kama ujasiri wake wa kukabiliana na Iran, matamshi yaliyoungwa Mkono na Saudi Arabia.
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa Marekani kwa sasa imetengwa zaidi.
''Kuna rais ambaye anaweza kufutilia mbali makubaliano ya kimataifa akiwa pekee?'', aliuliza.
''Tatizo ni kwamba haelewi kuwa makubaliano haya sio kati ya Iran na Marekani pekee''.
No comments:
Post a Comment