Mhubiri ambaye alitabiri kuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe angefariki siku ya Jumanne, kwa sasa anajaribu kujitetea kwa sababu utabiri wake haukutimia, akisema kuwa Mungu amebadilisha fikra zake.
"Sababu iliyosababisha Mungu kuhairisha hili, hakuniambia - kwa hivyo sijui ni kwa nini Mungu aliamua kuchukua mkondo huo. Ninajua watu wengi walikuwa wakitarajia kutimia kwa unabii kwa sababu ya kile kinachoendelea nchini mwetu."
Mhubiri huyo raia wa Zimbabwe Philip Mugadza alijaribu kuishawishi mahakama ya juu nchini humo kutupa kesi dhidi yake kwa kutabiri kuwa Rais Robert Mugabe, 93, angefariki tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 2017.
Kesi hiyo itarudi mahakamani ambapo mhubiii Mugadza - kiongozi wa kanisa la The Remnant ameshtakiwa.
Wakati wa kukamatwa kwake wakili wake Gift Mtisi aliiambia BBC kuwa "anakubali kusema hivyo. Anasema hakudanganya - huo ni ujumbe kutoka kwa Mungu. Polisi watahitaji kuthibitisha kuwa Mungu hakusema hilo."
Mawakiia wake pia waliitaka mahaka ya katiba kutupilia mbali mashtaka hayo kwa misingi kuwa yanakiuka haki yake ya uhuru wa kusema.
Mwendesha mashtaka anasema kuwa muhubiri huyo alitukana dini ya kikiristo na tamaduni za Afrika kwa kutabiri kifo cha Mugabe.
Kutabiri kifo cha kiongozi ni mwiko, kulingana na imani za kitamaduni.
No comments:
Post a Comment