Saturday, October 28

Marekani yamtaka Kabila kuitisha uchaguzi 2018

Ziara ya Balozi Nikki Haley DRC
Mjumbe maalum wa Marekani Nikki Haley amesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) lazima ifanye uchaguzi mwaka ujao kinyume cha hivyo haitopatiwa msaada wa kimataifa kuandaa uchaguzi huo.
Haley amesema hayo mapema Ijumaa mjini Kinshasa baada ya kukutana na maafisa wa uchaguzi Ijumaa.
“Tunataka kuwepo na uchaguzi huru na wa haki mwaka 2018 mapema kabisa, na siyo mwisho wa mwaka huo –tunataka ufanyike haraka kabisa,” amesema Haley.
Ametoa wito kwa Rais Joseph Kabila kutangaza kuwa uchaguzi utafanyika mwaka 2018.
DRC ilitakiwa kufanya uchaguzi mwaka 2016 lakini Rais Kabila alikataa kuondoka madarakani pamoja na kuwa muhula wake wa uongozi ulimalizika Disemba 2016.
Tume ya uchaguzi nchini humo imesema haitakuwa tayari kuandaa uchaguzi hadi April 2019. Upinzani unamshutumu Kabila kwa kujaribu kuvuta muda ilia pate fursa ya kubadalisha katiba na kuondoa ukomo wa muda wa kutumikia urais.
“Serikali ya Marekani haitosaidia kitu chochote kama uchaguzi utafanyika 2019. Jumuiya ya kimataifa haitosaidia kitu chochote mwaka 2019,” Haley alisema Ijumaa.

No comments:

Post a Comment