Tuesday, October 17

Mahakama: Mwenyekiti wa IEBC hana uwezo wa kurekebisha matokeo Kenya

Jaji mkuu David Maraga
Image captionJaji mkuu David Maraga
Mahakama ya upeo nchini Kenya imeunga mkono uamuzi wa mahakama ya rufaa unaomnyima uwezo mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kurekebisha matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo bunge.
Mahakama hiyo ya juu iliamua kwamba matokeo ya uchaguzi yaliotangazwa katika maeneo bunge ni ya mwisho.
FOMU 34
Katika uamuzi wa mwisho , majaji watano wa mahakama hiyo walisema kuwa kulikuwa na hitilafu kati ya matokeo ya fomu 34A na 34B, mwenyekiti anafaa kutangaza matokeo ya uchaguzi na kuwaachia mahakama swala hilo kuamua.
Majaji hao walisema kuwa bwana Chebukati ana wajibu wa kukagua matokeo hayo kama yalivyopeperushwa kwa njia ya kielektroniki.
Hatahivyo kila anapokumbana na hitilafu , anapaswa kuelezea vyama vilivyopo, wachunguzi wa uchaguzi na raia na kuwachia swala hilo mahakama ya uchaguzi.
Katika uamuzi uliosomwa na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ,mahakama ilisema kuwa uwezo wa mwenyekiti kuchunguza matokeo sio agizo lililotolewa na mahakama bali ni sheria iliopo katika katiba na sheria za uchaguzi.
Walisema kuwa ukaguzi huo ulilenga kuhakikisha kuna usahihi na kuzuia wizi wa kura.
Mahakama: Mwenyekiti wa IEBC hana uwezo wa kurekebisha matokeo Kenya
Image captionMahakama: Mwenyekiti wa IEBC hana uwezo wa kurekebisha matokeo Kenya
Jaji Jacton Ojwang alikuwa na uamuzi tofauti huku jaji David Maraga, Philomena Mwilu, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola wakitoa uamuzi wa wingi.
Kesi ya Kiai:
Katika kesi yake, tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC ilisema kuwa ombi hilo lilikuwa haliangazii uamuzi wa mahakama ya juu wa tarehe mosi mwezi Septemba.
Tume hiyo iliongezea kwamba ombi hilo sio rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa inayojulikana kama Kesi ya Maina Kiai, ilioamuru kwamba matokeo yatakayotangazwa katika vituo vya kupigia kura ndio matokeo ya mwisho.

No comments:

Post a Comment