Wednesday, October 11

Madaktari watangaza mgomo


Kampala, Uganda. Madaktari kupitia mwavuli wa chama chao (UMA) wamepiga kura kuamua kuitisha mgomo wa kazi katika hospitali zote za umma kuanzia mwezi ujao, ikiwa serikali haitatekeleza madai yao.
Orodha ya madai yao ni nyongeza ya posho zikiwemo za kazi muda wa ziada, nyumba, usafiri, kufanya kazi maeneo hatarishi na ada ya uhifadhi kazini.
Katika mkutano wa kawaida wa madaktari huo uliofanyika hospitali ya Mulago jijini Kampala Jumatatu, madaktari pia walipiga kura kuridhia mapendekezo ya mishahara na posho kwa matabibu. Ingawa walipiga kura kuanza mgomo mara moja, Profesa Francis Omaswa wa Jukwa la Tiba kwa Wazee na Mjumbe wa Kamati ya Bunge kuhusu Wafanyakazi Dk Sam Lyomoki walishauri tofauti.
Hiyo ilikuwa baada ya Rais wa UMA, Dk Ekwaro Obuku aliyepokewa kwa shangwe alipoingia kwenye mkutano huo, kuwataka wanachama wote kupiga kura kuamua mgomo ufanyike.
Isipokuwa daktari mmoja, madaktari wengine wote walipiga kura kuamua mgomo uanze Novemba 6.

No comments:

Post a Comment