Wednesday, October 11

Kiongozi Bavicha apata ajali ya gari


Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Edward Simbeye amepata ajali ya gari.
Simbeye alikuwa akitokea Dar es Salaam kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano asubuhi, Simbeye amesema ajali hiyo ilisababishwa na tairi la mbele kushoto kufyatuka hivyo gari kupoteza mwelekeo na kuanguka kando mwa barabara eneo la Kawawa mjini Moshi.
“Namshukuru Mungu nimetoka salama mimi na mdogo wangu… nilikuwa nakwenda nyumbani kwa sababu za kifamilia,” amesema Simbeye.

No comments:

Post a Comment