Monday, October 23

Jimmy Carter: Nitaenda Korea Kaskazini kwa niaba ya Trump

Jimmy CarterHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJimmy Carter
Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, amesema yuko tayari kwenda Korea Kaskazini, kwa niaba ya serikali ya Rais Trump, ili kwenda kuzima mvutano unaozidi.
Aliliambia gazeti la New York Times, kwamba amezungumza na Mshauri wa Rais Trump, anayehusika na Usalama wa taifa, Jenerali McMaster ambaye ni rafiki yake kuhusu swala hilo.
Bwana Carter, ambaye sasa ana miaka 93 alisema, serikali ya Marekani, inakisia vibaya kauli ya Uchina juu ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Alisema kauli ya uchina siyo kubwa hivyo, tofauti na hayati baba na babu wa Kim Jong Un, ambaye anafikiriwa hata hakuwahi kuzuru Beijing.

No comments:

Post a Comment