Wednesday, October 4

Filamu tarajiwa ya Oscar Pistorius yazua utata

filamu
Image captionOscar Pistorius akiwa mwanariadha wa nchini Afrika Kusini
Familia ya mwanariadha mlemavu wa miguu kutoka nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyefungwa kwa kosa la kumuua mpenzi wake. Reeva Steenkamp imetoa tamko lenye nia ya kwenda mahakamani kufuatia kusudio la watengeneza filamu inayohusu maisha ya mwanariadha huyo .
Filamu hiyo, iliyopewa jina la Blade Runner Killer,, inayotarajiwa kutolewa nchini Marekani mwezi ujao.
Familia ya mwanariadha huyo inasema kwamba huo ni uwazi mbaya kabisa wa ukweli.
Nayo familia ya marehemu Steenkamp imekinza madai hayo kwamba hadithi ama maudhui ni kutokana na mtazamo wa Reeva na mama yake.

No comments:

Post a Comment