Tuesday, October 17

DRC yapewa kiti kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu

media
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imepewa kiti Jumatatu katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Oktoba 16, 2017. 2017.
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa umetoa idhni kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu. DRC ingelipata kura angalau 97. Lakini ilipata kura 151. Kwa kura hizo inakua moja kwa moja na moja ya viti vilivyohifadhiwa kwa kundi la nchi za Afrika.
Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu lilirejelea upya viti vinne vinavyohifadhiwa kwa kundi la nchi za Afrika, na DRC ilishinda kwa wingi wa kura, licha ya kampeni ya wanaharakati wa DRC ambao walikua wametoa wito wa kuizuia Kinshasa kupata nafasi hiyo kutokana na ukiukwaji mkubwa unaoendelea kutekelezwa na serikali kupitia maafisa wake mbalimbali, wanaharakati hao wamesema.
Ili kupata idadi kubwa kabisa katika Mkutano Mkuu, DRC ilihitaji tu msaada wa nchi 97. Ilipata zaidi ya kura hizo kwa sababu nchi 151 zilipigia kura.
Hata hivyo, wagombea wengine watatu kutoka Afrika - Senegal, Nigeria na Angola - walichaguliwa kwa kura nyingi.
Haitatambulika, hata hivyo, nchi ambazo zilipigia kura DRC kwa sababu kura ilikua ya siri.
Kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2020, DRC itashiriki vikao vya Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, ambalo hivi karibuni lilianzisha uchunguzi nchini DRC kufuatia vurugu katika jimbo la Kasai.
Kwa upande wa serikali ya DRCongo, ambao ilitumia muda mrefu kwa kuendesha kampeni ya kupewa kiti hicho, imesema, imepata ushindi mkubwa. Waziri wa Haki za Binadamu pia amekaribisha ushindi huo kwenye Twitter. 
Kwa upande wa watetezi wa haki za binadamu, hata hivyo, wanasema wameangushwa. Mashirika 157 ya haki za binadamu kutoka DRCyalikua yalitoa wito kwa wanachama wa Umoja wa Mataifa kupiga kura dhidi ya DRC kwa sababu ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliongezeka tangu mwaka uliopita.
Philippe Bolopion, msemaji wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch mjini New York, amekasirika kuona DRC imejiunga na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.
Marekani imehtumu kura hiyo. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, amesema uchaguzi wa DRC unaonyesha jinsi gani Baraza la Haki za Binadamu limepoteza "uaminifu" wake.
Kwa upande wa Lambert Mende, msemaji wa serikali ya DRC, kuchaguliwa kwa DRC ni "ishara ya huruma" kwa jumuiya ya kimataifa.
Balozi wa Uingereza, Matthew Rycroft, amesema kuchaguliwa kwa DRC ni jambo ambalo "linakatisha tamaa".

No comments:

Post a Comment