Thursday, October 5

Diamond afikishwa mahakamani kwa matunzo ya mtoto


Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
Wakili Zulu akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto  (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment