Wednesday, October 11

DC ARUSHA MJINI AWATAKA WANANCHI KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA


 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo.
 Akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Tanzania kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha Daqqaro, amesema kuwa zoezi hili lina manufaa makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujumla lakini pia vitambulisho hivyo vitawawezesha watanzania kutambulika kila mahala, pamoja na raia wa kigeni kufanya shughuli zao bila usumbufu ikiwa ni pamoja serikali kuwa na taarifa sahihi za wananchi.
 Aidha amesema kuwa wananchi wasisubiri mpaka zoezi hilo kufikia tamati ndio kujitokeza Kwa wingi  kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano na usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Naomba niwafahamishe na kutoa rai kwa wananchi wangu wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili na wasisibirie siku kubaki chache ndio wajitokeze kwa kuwa kunapelekea usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi”alisema fabian

 Pia ametaka kila mwananchi kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala ya kisiasa kutokana na umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na kusajili na kutoa vitambulisho vya taifa.

Afisa kutoka mamlaka hiyo wilaya ya Arusha Mjini  Juliette Raymond  Amesema lengo la zoezi hilo ni kuwezesha serikali kutambua wananchi wake wapo wapi na wanafanya nini ilimradi  anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania ,hivyo zoezi hilo ni  lazima kwa kila mtu kwa Mujibu wa sheria.

Kwa wilaya ya Arusha Mjini zoezi hilo linaendelea katika kata ya Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi hilo linafnyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kata ya Sekei,Themi katika viwanja vya nane nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji kata eneo la Mbauda Sokoni.

No comments:

Post a Comment