Wednesday, October 25

Dareva wa naibu jaji mkuu apigwa risasi Kenya

Dereva wake amepigwa risasi na kujeruhiwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNaibu jaji Mkuu wa Kenya Philomena Mwilu
Dereva wa naibu jaji mkuu wa Kenya Philomena Mwilu amepigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana mjini Nairobi.
Dereva huyo anayejulikana kama afisa wa polisi Titus Musyoka alipigwa risasi nje ya jumba la Marsabit Plaza katika barabara ya Ngong.
Afisa mkuu wa polisi eneo la Dagoretti Rashid Mohammed alisema kuwa kisa hicho kilitokea mwendo wa saa kumi na nusu jioni na jaji Mwilu hakuwepo katika gari hilo.
Alisema kuwa dereva aliyejeruhiwa alipigwa risasi katika bega na anapatiwa matibabu katika hospitali moja ya mjini Nairobi.
Amesema kuwa maafisa wa polisi wanakichukulia kisa hicho kuwa cha ujambazi lakini uchunguzi unaendelea.
Tayari maafisa wa uchunguzi wamefika katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment