Tuesday, October 3

Chuo cha Nairobi chafungwa kwa sababu za kiusalama

Polisi wakimtia mbaroni mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakiandamana kushinikiza kuachiliwa huru kwa Babu Owino Alhamisi wiki iliyopitaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionBaadhi ya wanafunzi wa chuo cha Nairobi waliandamana kushinikiza kuachiliwa huru kwa Babu Owino Alhamisi wiki iliyopita
Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya kile ambacho viongozi wa chuo hicho wamesema ni haja "kudorora kwa usalama" chuoni humo.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya siku kadha za wasiwasi uliotokana na makabiliano kati ya wanafunzi na polisi wa kukabiliana na fujo ndani ya chuo hicho.
"Wanafunzi wote wametakiwa kuondoka vyumba vyao vya malazi mara moja kabla ya saa tatu asubuhi," taarifa ya seneti ya chuo hicho imesema.
Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino.
Bw Owino, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.
Baadaye alikamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mengine ya kumshambulia mpiga kura wakati wa uchaguzi mwezi Agosti.
Aliachiliwa kwa dhamana.
Wanafunzi takriban 26 walijeruhiwa. Video ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni zimeonyesha maafisa wa polisi wakiwafurusha wanafunzi kutoka kwa vyumba vya malazi na hata kwenye madarasa.
Polisi na wanafunziHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionPolisi wakiwa kwenye wakiwa mkabala na wanafunzi waliokuwa wakiandamana chuoni
Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema kufikia sasa ni vigumu kubaini iwapo video hizo ni za kweli na iwapo wanaoonekana wakipigwa na maafisa wa polisi ni wanafunzi.
Mamlaka inayosimamia utendakazi wa polisi na kutetea haki za raia (IPOA) imetoa wito kwa wanafunzi 26 ambao walijeruhiwa kuandikisha taarifa.
Mwanafunzi akitiwa mbaroniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
"Kuandikishwa kwa taarifa hizi kutatusaidia kuharakisha uchunguzi," taarifa ya IPOA iliyotiwa saini na afisa mkuu mtendaji Dkt Joel Mabonga imesema.
Awali, taarifa ya mwenyekiti wa IPOA Macharia Njeru ilikuwa imesema: "Ni kweli wapo wanafunzi ambao walijeruhiwa na baadhi ya maafisa wa polisi walipokuwa wanakabiliana na waandamanaji. Kufikia sasa, hatujapokea ushahidi wowote wa kuonesha kunaye aliyefariki."
Bw Njeru alisema baada ya uchunguzi, wamebaini nyingi za video na picha ambazo zinaenezwa mtandaoni zikidaiwa kuwaonesha polisi wakiwashambulia wanafunzi ni za uzushi.

No comments:

Post a Comment