Chama kimoja cha siasa nchini New Zealand kimeamrishwa na mahakama kulipa dola 412,000 kwenye kesi iliyowasilishwa na mwanamuziki raia wa Marekani Eminem.
Chama cha National Party, kilitumia mdundo wenye sauti sawa na wimbo wa Eminem wa Lose Yourself, katika matangazo yake ya uchaguzi.
Wimbo huo kwa jina Eminem-esque ulikuwa na tofauti kidogo na wimbo wake Eminem.
Kesi hiyo iliyoanza mwezi Mei ndiyo ya hivi punde kuhusu midundo inayofanana na muziki halali.
- Wasanii na wachezaji matajiri zaidi duniani watajwa
- Facebook yanunua app ya vijana
- Justin Bieber apigwa marufuku China
Wachapishaji wa nyimbo za Eminem Eight Mile Style, walipeka kesi mahakamani baada ya chama cha National Party, kutumia mdudo wa wimbo huo ulioshinda tuzo ya Oscar katika kampeni yake mwaka 2014.
Mawakili wa chama walisema kuwa mdundo uliotumiwa haukuwa wa wimbo wa Lose Yourself, lakini wimbo unaojulikana kama Eminem-esque, ambao waliununua kutoka maktaba ya muziki.
Hata hivyo mahakama iliamua siku ya Jumatano kuwa mdundo huo ulifanana na wimbo wa Eminem.
No comments:
Post a Comment