BAADA ya kusambaa kwa picha za mwanamitindo Calisah Abdulhameed, akiwa amevaa viatu vya kike (High Heels), modo huyo amefunguka kuwa licha ya kitendo hicho kupokewa na jamii kwa mitazamo tofauti malengo ya kutangaza bidhaa hiyo yametimia.
Akizungumza na MTANZANIA, Calisah alisema kwa mara ya kwanza alipopigiwa simu na jamaa anayeitwa Frank Knows anayewavalisha viatu mastaa wa kike kama, Jokate Mwegelo na Hamisa Mobetto ili afanye tangazo hilo alisita lakini baadaye alikubali baada ya kulipwa dau kubwa alilolitaka.
“Frank Knows tayari amewavisha kina Jokate na Hamisa Mobetto lakini alikuwa hafahamiki sana ila nilipovivaa mimi vile viatu watu wengi wamemfahamu na kiukweli mpango wa biashara yake umefanikiwa, nimepokea matusi mengi lakini ukweli ile ni kazi tu na mimi ni mwanamume kamili, nisihisiwe vibaya,” alisema Calisah.
Modo huyo ambaye alijizolea umaarufu mwaka jana baada ya kutoka kimapenzi na Wema Sepetu aliongeza kuwa mashabiki wa mitindo wataelewa zaidi baada ya tangazo la video kuanza kuonekana kupitia runinga zote.
No comments:
Post a Comment