Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imeanza kuwatembelea wateja wake katika maeneo yao ya kazi ili kusikiliza kwa ukaribu changamoto wanazokutana nazo zinazohusu huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kuwa wateja wake.
Aidha, katika wiki hii ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imemtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Azania Bank Limited, Ndugu Charles Jackson Itembe, ambaye pia ameongoza msafara wa kutembelea wateja katika maeneo yao ya kazi, ambapo mteja aliyetembelewa leo na Benki hiyo, Ndugu Augustine Nyato amekabidhiwa hati ya kuthaminiwa pamoja na biashara ya mteja huyo kuwa katika biashara watakazozipa kipaumbele.
Akizungumza na mteja huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe amesema ikiwa Azania Benki inamjali mteja wameamua kuwatembelea wateja wadogo, wa kati na wakubwa ili kuwapa shukrani kwa kuendelea kuwa na wao katika biashara kwa kipindi kirefu na hata kwa kipindi kijacho ili kunafaika na benki hiyo.
Naye Mteja huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Israel Aaron & Company Augustine Nyato ameishukuru benki ya Azania kwa kutambua mchango mkubwa wa wateja wao mpaka wakaamua kumtembelea ili kusikiliza changamoto anazozipata katika benki hiyo pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana vyema katika kutoa huduma iliyobora ili kufikia malengo aliyojiwekea.
Wiki ya huduma kwa wateja imeanza rasmi Jumatatu ya Oktoba 2, 2017 na itamalizika baada ya wiki moja. Ni wakati wa taasisi kuwa karibu zaidi na wateja wake. Ni wakati wa kwenda bega kwa bega katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na mteja wa benki ya Azania ambaye ni mfanyabiashara na mkurugenzi wa Israel Aaron & Company Augustine Nyato kuhusu benki hiyo ilivyoamua kuwatembelea wateja wake katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) akimkabidhi hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania, Bwana Augustine Nyato leo ofisini kwake katika mtaa wa Survey jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Tawi wa Benki ya Azania Tawi la Masdo, Benson Msuya.
Mteja wa Banki ya Azania bwana Augustine Nyato( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto), Meneja wa Tawi wa Benki ya Azania Tawi la Masdo, Benson Msuya(wa pili kutoa kulia) na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia).
No comments:
Post a Comment