Wednesday, October 25

Barua ya mwanafisikia kuhusu furaha yauzwa dola milioni 1.5

Gal Winner, owner and manager of the Winner's auction house in Jerusalem, displays two notes written by Albert Einstein, in 1922, on hotel stationary from the Imperial Hotel in Tokyo (22 October 2017)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionEinstein alipeana barua hizo kwa msafirishaji mmoja wa mizigo mjini Tokyo mwaka 1922 badala ya zawadi ya pesa.
Barua mbili za Albert Einstein zianazoeleezea falsafa yake kuhusu kuishi maisha ya furaha, zimeuzwa kweenyr soko la mnada mjini Jerusalem kwa dola milioni 1.56.
Einstein alipeana barua hizo kwa msafirishaji mmoja wa mizigo mjini Tokyo mwaka 1922 badala ya zawadi ya pesa.
Alikuwa amesikia habari kuwa alikuwa ameshinda tuzo na kumuambia msafirishaji huyo wa mizigo kuwa, kama angekuwa na bahati baraua hizo zingekuwa na umuhimu sana.
Einstein alisema kwenye barua hizo kuwa kutimiza lengo la muda mrefu halileti fuuraha wakati wote.
Mwanafisikia huyo mzaliwa wa Ujerumani alikuwa ameshinda tuzo la Nobel la fisikia na wakati huo alikuwa ziarani nchini Japan.
German-born Swiss-US physicist Albert Einstein in Princeton (14 February 1950)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEinstein (katika picha ya mwaka 1950)
Wakati msafirishaji wa mizigo alifika kwenye chumba chake Einstein hakuwa na zawadi ya pesa kumpta.
Badala yake alimpa mtu huyo ujumbe aliokuwa ameuweka sahihi yake akitumia karatasi ya hoteli ya Imperial ya mjini Tokyo. Ujumbe kwenye baru hiyo iliyokuwa imeandikwa kwa lugha ya kijerumani ulisema; "Maisha ya utulivu yataleta furaha nyingi kuliko kutafuta mafanikio na ukosefu wa utulivu unaoambatana nao."
Inaripotiwa kuwa mmoja wa wanunuzi wa barua hizo ni kutoka barani Ulaya na kwamba hangependa kutajwa jina.
Muuzaji anatajwa kuwa mpwa wa msafirishaji mizigo.

No comments:

Post a Comment