Shehena ya Almasi iliokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Ambayo jana ilioyeshwa hadharani wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na viongozi wegine wa Serikali, alipokwenda kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa madini hayo kiwanjani hapo jana. Picha na Ikulu
Watuhumiwa hao walikamatwa na mzigo huo ambao ulizuliwa na Serikali ili ufanyiwe tathimini upya kujua thamani halisi baada ya thamani iliyotumika kutiliwa mashaka na Serikali.
Jeshi la polisi liliwashikilia watuhumiwa wanne kwa uchunguzi na hatua nyingine za kisheria baada ya kuzuia mzigo huo.
Mzigo huo wa almasi ulikuwa unatoka mgodi wa Mwadui ambao ni wa ubia kati ya Serikali na kampuni ya Petra Diamonds ya Afrika Kusini kwa hisa 25 za Serikali na Petra Diamonds hisa 75.
No comments:
Post a Comment