Tuesday, September 12

Upelelezi kesi dhidi ya Halima Mdee wakamilika




Dar es salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Oktoba 11 kumsomea maelezo ya awali Mbunge wa Kawe (Chedema), Halima Mdee.
Mbunge huyo anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa amesema upelelezi wa kesi umekamilika, hivyo kuomba shauri hilo lipangiwe tarehe kwa ajili ya kumsomewa mshtakiwa maelezo ya awali.
Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11.
Mdee anakabiliwa na shtaka la moja la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 4 makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Anadaiwa kutamka kuwa Rais anazungumza  ovyo ovyo na anatakiwa afungwe break, kauli inayodaiwa ingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment