Msigwa aliyekuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema waliomsafirisha Lissu kutoka Dodoma siku hiyo kwenda jijini Nairobi, aliliambia gazeti hili jana kwamba Lissu alivuja damu nyingi na kama asingepata huduma ya haraka angefariki.
“Tulipofika Nairobi, madaktari walishangaa kuona Lissu akiwa hai, kwa sababu alipoteza damu nyingi sana. Lakini niwashukuru sana madaktari wa hospitali ya Dodoma General kwa huduma waliyotoa kufanya Lissu tufike Nairobi,” amesema Mchungaji Msigwa na kuongeza:
“Nataka tu niwaambie Watanzania kwamba Tundu Lissu wetu aliumizwa sana katika jaribio la kuchukua uhai wake. Watu wasichukulie kama ni jambo dogo, ni jambo kubwa lililoharibu hata akili za watu tuliokuwa karibu naye.” Soma Zaidi
No comments:
Post a Comment