Friday, September 1

Maabara sita za kanda kuimarishwa

Kaimu meneja masoko, mawasiliano na huduma kwa

Kaimu meneja masoko, mawasiliano na huduma kwa wateja  ,Cletus Mnzava 
Dar es Salaam. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema  inalenga kuimarisha maabara sita za kanda nchini.
Cletus Mnzava, ambaye ni kaimu meneja masoko, mawasiliano na huduma kwa wateja  wa mamlaka hiyo, amesema kanda hizo ni ya Ziwa inayohudumia mikoa ya Mwanza, Kagera, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kigoma.
Zingine ni kanda za Kaskazini, Kati, Mashariki, Nyanda za Juu Kusini na ya Kusini.
Amesema wanakusudia kuimarisha utendaji kazi wa kanda hizo kwa kuzipatia vifaa vya maabara vya kisasa.
Mnzava amesema huduma za kimaabara zimeboreshwa hivyo wananchi wazitumie walipo.
Kaimu meneja masoko huyo amesema wapo baadhi ya watu ambao wanashindwa kupata huduma za kimaabara maeneo ya karibu kwa sababu ya mazoea, hivyo kutumia gharama kubwa kusafiri kuzifuata Dar es Salaam.
Amesema mkakati uliopo ni wa kuanza ujenzi wa ofisi za kanda ili kuondokana na kero wanayopata ya kuhamahama inayosababisha upotevu wa vifaa.

No comments:

Post a Comment