Thursday, September 14

Kubenea augua ghafla, apumzishwa hospitali Dom


Dodoma. Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea ameugua ghafla na kupumzishwa katika zahanati ya Bunge.
Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Alhamisi jioni kuwa mbunge huyo alikwenda katika zahanati hiyo baada ya kujisikia vibaya.
“Alijisikia kukosa nguvu akaenda katika zahanati hiyo, amepumzishwa na sasa hivi ndio anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu apumzishwe. Ndio kwanza amekaribia kumalizia dripu,” amesema Silinde.
Hata hivyo waandishi wa habari walipofika katika zahanati hiyo hawakuruhusiwa kumuona na badala yake wauguzi walisema amepumzika.
Daktari wa zahanati ya Bunge, Dk Noel Solomoni amethibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo  tangu saa 10 jioni leo.
Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza zaidi kama alifikishwa ama alikwenda mwenyewe katika zahanati hiyo iliyopo ndani ya Bunge.

No comments:

Post a Comment