Wednesday, September 27

Kile unachohitaji kufahamu kuhusu Korea Kaskazini

Huku Korea Kaskazini na Marekani wakiendelra kurushiana vitisho, hatufahamu vile vita hivyo vya maneno vinavyopokelewa na watu wa Korea Kaskazini kwa sababu utawala wa nchi hiyo umewafungui kabisa watu wake na kuwazui na mambo yanayojiri sehemu zingine za dunia.
Ni vigumu kupata takwimu zozote kutoka nchi hiyo lakani makadirio tofauti yanatuambia nini kuhusu maisha yalivyo nchini Korea Kaskani?
Utawala wa kiimla dhidi ya Demokrasia
Kim Il-sung alianzisha Korea Kaskazini mwaka 1948 na familia yake imetawala nchi tangu wakati huo
Image captionKim Il-sung alianzisha Korea Kaskazini mwaka 1948 na familia yake imetawala nchi tangu wakati huo
Kim Il-sung alianzisha Korea Kaskazini mwaka 1948 na familia yake imetawala nchi tangu wakati huo na mamlaka imetoka kwa baba kweda kwa mtoto.
Katika kipindi kama hicho korea kaskazini imepitia jamhuri 12, mapinduzi kadha na mabadiliko kwenda kwa uchaguzi ulio huru na wa haki.
Kwa ujumla marais 12 wameiongoza nchi kwa jumla ya mihula 19 ofisini.
Watu wachache wana simu za mkononi
Wamiliki wa siku kati ya Korea Kaskazini na Kusini
Image captionWamiliki wa siku kati ya Korea Kaskazini na Kusini
Simu za mkononi milioni 3 zinaweza kuonekana kuwa nyingi zaidi lakini kwa nchi yenye watu milioni 25 hii ni sawa na mtu mmoja kati ya watu 10 walio na simu .
Wengi wa wake walio na simu huenda wako kwenye mji mkuu Pyongyang
Kinyume na nchini Korea Kusini yenye watu milioni 51, kuna simu nyini kuliko watu.
Watu wa Korea Kaskazini ni wafupi kuliko watu wa Korea Kusini
Korea Kaskazini wana kimo kifupi kuliko Korea Kusini
Image captionKorea Kaskazini wana kimo kifupi kuliko Korea Kusini
Inaweza kuonekana kama hadithi tu lakini utafiti unaonyesha kuwa watu wa Korea Kaskazini wana kimo kifupi kuliko wale wa Korea Kusini.
Professor Daniel Schwekendiek kutoka chuo cha Sungkyunkwan mjini Seol, alichunguza kimo cha wakimbizi wa Korea Kaskazini waliopimwa baada ya kuvuka mpaka na kuingia Korea Kusini na kupata kuwa kuna tofauti ya sentimita 3-8.
Uhaba wa chakula unatajwa kuwa sababu kuu ya watu wa Korea Kaskazini kuwa na kimo kifupi.
Barabara za Korea Kaskazini ni mbaya
Barabara za Korea Kaskazini na Korea Kusini
Image captionBarabara za Korea Kaskazini na Korea Kusini
Picha kutoka mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang mara nyingi huonyesha barabara pana zisizo na magari lakini nje ya mji ni hali tofauti.
Korea Kaskazini ina jumla ya kilomita 25,554 za barabara lakini takwimu za mwaka 2006, lakini ni asilimia 3 tu ya barabara hizo zilizo la lami ikiwa ni kama kilomita 724 tu.
Pia inasemekana kuwa ni watu11 kati ya watu 1,000 nchini Korea Kaskazini wanaomiliki gari.
Bus queue in North KoreaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUsafiri wa umma ni mbaya Korea Kaskazini
Tegemeo kuu kwa uchumi nchini Korea Kaskazini ni mkaa wa mawe
Asilimia kubwa na mkaa wa Korea Kaskania huuzwa nchini China
Image captionAsilimia kubwa na mkaa wa Korea Kaskania huuzwa nchini China
Korea Kaskazini inategemeaa mauzo ya mkaa wa mawe kwa uchumi wake. Lakini ni vigumu kufahamu thamani yake kwa sababu data hutoka kwenye nchi zinazonunua bidhaa hizo.
Asilimia kubwa na mkaa wa Korea Kaskania huuzwa nchini China, ambayo ilipiga marufuku bidhaa hiyo mwezi Februari 2017.
Hata hivyo meli za Korea
Hata hivyo meli za Korea Kaskazini zimeonekana kutia nanga kwenye bandari za mkaa wa mawe nchini China.
Ubabe wa kijeshi
Ubabe wa kijeshi
Image captionUbabe wa kijeshi
Hukun Korea Kaskania ikiwa nchi ya 52 wa idia ya watu dunaia, inatajkwa kuwa katika nafai ya ne kati ya nchi zilio na jeshi kubwa zaiid dunaini.
Matumizi ya jeshi yanatajwa kuchukua asilimia 25 ya pato lote la nchi, na karibu kila mwanamme nchini Korea Kaskazini hupitia mafunzo fulani ya kijeshi
Watu nchini Korea Kusini huishi miaka mingi
Miaka ya kuishi
Image captionMiaka ya kuishi
Majanga ya njaa miaka ya 1990 yalisababisha kushuka kwa miaka ya kuishi nchini Korea Kaskazini, lakini hata bila ya hilo miaka ya kuishi nchini Korea Kaskazini inapungua kwa miaka 12.
Kuna uhaba wa chakula na hii ni moja sabubau nyingi ya sababu ambazo husababisha watu kuishi miaka mingi nchini Korea Kusini.

No comments:

Post a Comment