Jana ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kuelezea mchakato wa utumaji wa fedha hizo kiasi cha Sh 43 milioni ikisema kuwa zilitumwa tangu Agosti 20. Ofisi hiyo ilikuwa ikifafanua taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyewaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa hajapa mchango huo wa wabunge.
Ali aliyepo Nairobi amesema amethibitishiwa na Hospitali ya Nairobi kupokea fedha hizo kutokaTanzania ingawa kulikuwa hakuna maelezo zaidi.
“Wamenieleza kuna fedha zimeingizwa kutoka Tanzania ila hazina maelezo ndiyo wanafuatilia benki,” amesema ofisa huyo.
No comments:
Post a Comment