Facebook itaongeza uangalizi zaidi wa binadamu katika mfumo wake wa matangazo ya biashara baada ya kukiri kwamba ilishindwa kuzuwia, wala hata kutambua, walengwa wa chuki dhidi ya wayahudi kwenye mtandao wake.
Afisa Mkuu wa shughuli za mtandao wa Facebook Sheryl Sandberg, amesema kuwa "aligadhabishwa" na matokeo ya uchunguzi wa kampuni ya ProPublica yaliyochapishwa wiki iliyopita.
Ripoti hiyo ilibaini kuwa matangazo ya biashara huenda yananunuliwa na watu wanaolengwa pekee ambao wanaojielezea kama "watu wanaochukia wayahudi ", pamoja na maneno mengine ya aina hiyo ya chuki.
"hatukulenga ama kutarajia huduma hii itatumiwa hivi - na hilo ni jukumu letu ," aliandika Bi Sandberg.
Katika taarifa hiyo iliyotumwa kwenye Facebook, aliongeza kuwa: "kuona maneno hayo nilihisi kukasirika na kukata tamaa - kukasilishwa na hisia hizi za chuki na nivunjika moya kwamba mifumo yetu iliruhusu hili kufanyika.
"chuki haina nafasi kwenye Facebook - na kama Muyahudi, kama mwanamke na , kama binadamu, nafahamu athari zinazoweza kutokana na chuki.
"Ukweli kwamba maneno ya chuki yalikuwa yakitumiwa kama maneno mtu anayoweza kuchagua kuyatumia halikuwa jambo sahihi na nakiri kuwa yalikuwa mapungufu upande wetu.
Tuliyaondoa na pale ambapo hilo halitafanikiwa , tutaondoa kipengele kinachowezesha kuwalenga watu katika mifumo yetu ya matangazo ya biashara."
Zaidi ya hayo Bi Sandberg alisema kuwa Kampuni ya Facebook inatengeneza mfumo mpya ambao unaweza kuwaruhusu watumiaji wa mtandao huo kuripoti matangazo ya biashara ambayo hayafai, sawa na vile mtu ambavyo unaweza kuripoti ujumbe usiofaa kwa sasa kwenye ukurasa wako.
Facebook sio kampuni pekee ya mtandao iliyojipata kataika athari za mfumo duni wa kudhibiti matangazo ya biashara yasiyofaa katika miezi ya hivi karibuni.
Kampuni ya Google pia ilitakiwa kuchukua hatua baada ya mfumo wake kuruhusu watumiaji kuweza kusaka taarifa za ubaguzi wa rangi na matamshi ya chuki dhidi ya wayahudi.
Mtandao wa Twitter pia ulilazimika kuchukua hatua kama hizo dhidi ya matumizi mabaya dhidi ya mfumo wake wa matangazo ya biashara.
No comments:
Post a Comment