Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
CHUO Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili kupitia Shule ya Famasi kwa kushirikiana kwa Kituo cha cha Mafunzo ya kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki wameendesha mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi. Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema mfumo wa kutathimini dawa za Afrika Mashariki ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa ukanda huo wanapata dawa bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.
Dk. Mpoki amesema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo kwa wataalam wa dawa wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki yanalenga kuhakikisha kuwa dawa zote zilizokidhi vigezo zinasajiliwa kwa mfumo wa ulinganifu unaotumika baada wataalam hao kujiridhisha kisayansi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu na wananchi katika utoaji wa taarifa pale wanapoona kuna dawa zenye mashaka ziko mtaani, hivyo kusaidia katika dhima ya kulinda afya ya jamii.
Amesema kuwa kuanzishwa kituo cha kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki kitakuwa ni msaada mkubwa katika kuhakikisha kuwa kila dawa zilizo katika nchi za Afrika Mashariki ni zile zilizosajiliwa na usajili huo ni kwa matumizi ya wananchi wote wa ukanda husika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki yalifanyika jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, Kulia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali wa MUHAS, Profesa Mainen Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi, Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akiwa katika pamoja na Maprofesa wa Chuo cha Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi pamoja na Watalaam jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment