Tuesday, September 5

Colombia kusitisha mapigano na waasi wa ELN

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu kwenye mji mkuu wa Equador, Quito
Image captionMakubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu kwenye mji mkuu wa Equador, Quito
Serikali ya Colombia na kundi la pili kwa ukubwa la waasi nchini humo, la ELN, wamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda.
Hatua hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika, inatarajiwa kuanza tarehe moja mwezi wa Oktoba na kuendelea kwa siku mia moja na mbili, lakini Rais Juan Manuel Santos amesema makubaliano hayo yanaweza kusogezwa mbele iwapo hayatakiukwa na iwapo kutakuwa na maendeleo katika mazungumzo ya amani.
Tangazo hilo limetolewa siku mbili kabla ya ziara ya Papa Mtakatifu nchini Colombia.
Rais Juan Manuel Santos amesema makubaliano hayo yanaweza kusogezwa mbele iwapo hayatakiukwa
Image captionRais Juan Manuel Santos amesema makubaliano hayo yanaweza kusogezwa mbele iwapo hayatakiukwa
Bwana Santos amesema nchi yake itafikia hatua muhimu katika historia.
Kundi la waasi la ELN, ni kama kundi kubwa la waasi la FARC ambalo limekuwa likipigana na serikali kwa zaidi ya nusu karne.

No comments:

Post a Comment