Utafiti uliofanywa na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) umeonyesha asilimia 62 ya wahojiwa hawafahamu kama wanatakiwa kutoa taarifa polisi wakipoteza laini.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo mjumbe wa baraza hilo Nyanda Shuli amesema wahojiwa wengi hawafahamu kama wanawajibika kuripoti taarifa hiyo.
Sanjari na hilo Shuli amesema asilimia 62 ya wahojiwa wameonyesha kutoelewa kwamba si sahihi kutumia laini iliyotumiwa awali na mtu mwingine.
"Yapo madhara ya mtu kutumia laini ya mtu mwingine au kushindwa kutoa taarifa ikipotea, hii inaweza kuhusishwa na uhalifu endapo itafika kwa mtu asiye na nia njema. Tumegundua wengi hawaelewi hilo, " amesema
No comments:
Post a Comment