Viongozi wa upinzani na wanaharakati wa haki za binaadam nchini Togo wametaka kuundwa kwa tume huru itakayochunguza mauaji ya watu wawili yaliyotokea wakati wa maandamano nchini humo.
Upinzani unasema kwamba watu saba waliuawa.
Serikali kwa upande wake inasema takriban maafisa sitini wa jeshi la polisi walijeruhiwa

Upinzani nchini Togo uliitisha maandamano hayo ambayo yalitaka kufuatwa kwa katiba ya mwaka 1992 iliyoweka ukomo wa uongozi wa Rais.
No comments:
Post a Comment